VYANZO VYA MATESO SAUDI ARABIA

 VYANZO VYA  MATESO SAUDI ARABIA 

Kwa mda wa miaka kadhaa,kazi za uarabuni zimekuwa zikiwavutia wasichana sio tu humu nchini Bali pia wale wa mataifa mengi na ni kazi ambazo wengi waliona zitawapiga jeki katika kukabiliana na makali ya maisha

Wale ambao hutafta kazi hizo za uarabuni,hutumia mawakala ambao huwaunganisha na waajiri.Baadhi ya mawakala hao wamesajiliwa ilhali hufanya shughuli hiyo kinyume na sheria.Hivo wakati mwingine kwa wasichana Hawa huwa vigumu kubainisha mawakala walioidhinishwa na wale bandia

Visa vingi vimeripotiwa hapa nchini vya wasichana kutoweka punde tuu wapoelekea uarabuni kwa kazi tofauti.Baadhi ya vidosho hao hurejeshwa humu nyumbani wakiwa mahututi na wengine wakiwa wamefariki

Licha ya serikali kwa mda mrefu kuwa kimya kuhusiana na changamoto wanazokumbana nazo wasichana wegi ughaibuni wito umekuwa ukitolewa kwa serikali kubainisha mchakato wa wakenya wanaotafta kazi katika mataifa haya

Aidha mawakala bandia wakusafirisha wakenya kuelekea katika mataifa ya kiarabu kufanya kazi ndio chanzo kinachotajwa kwa wakenya wanaoenda kwenye milki hizo za kiarabu

Akizungumza afisa wa maswala ya dharura katika shirika la kutetea haki za binadamu la MUHURI Francis Auma amesema hali ya mawakala ghushi imechangia pakubwa Hilo akiulaumu ubalozi wa Kenya nchini Saudi Arabia kwa kutotilia maanani mateso wanayopitia wakenya kwenye taifa hilo

Auma ameitaka serikali kupitia wizara ya maswala ya nchi za kigeni kuja na suluhu mwafaka ya kuhakikisha wakenya wanakua na usalama wanapokwenda kufanya kazi katika nchi hizo akisema kutowahakikishia usalama wa kikazi wakenya pia inachangia kwa waajiri wao kuzidi kuwanyanyasa


MHARIRI;LYDIA  ANN  

Comments

  1. Marvellous ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  2. ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  3. Good ๐Ÿ‘๐Ÿ˜Š

    ReplyDelete
  4. Nice work madam Lydia ๐Ÿ‘๐Ÿ‘keep it up

    ReplyDelete
  5. Swadakta ๐Ÿ‘ kazi safi Lydia keep it up ๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  6. Nice work,,kongole Kwa kazi njema

    ReplyDelete
  7. Good work sister ๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  8. Hili Hunijumbusha Rafki Yangu Bado Yuko Hizi Sehemu ๐Ÿ˜ข

    ReplyDelete
  9. Good job..keep it up๐Ÿ™๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  10. Amazing ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CHANGE MUST COME BUT MUST BE LED BY THE YOUTH

DEATH RATE INCREASES IN UNIVERSITIES

IF HUMANS CAN SLIGHTLY AMEND THEIR BEHAVIOURS